top of page

Taifa la Sudan Kusini lavamiwa na nzige wa jangwani wanaosababisha uharibifu mkubwa Afrika Mashariki

Kulingana na serikali ya Sudan Kusini, nzige hao wamevamia Kaunti ya Magwi Kusini inayopakana na taifa la Uganda.


Wizara ya kilimo nchini Sudan Kusini imesema kwamba kimbunga cha nzige wa jangwani wanaovamia mimea na maeneo ya malisho katika kanda ya Afrika Masharika kimeshuhudiwa nchini humo. Taifa la Sudan Kusini linakumbwa na hali ngumu ya ukosefu wa chakula na miaka mingi ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.


Nzige hao wamevamia Kaunti ya Magwi Kusini inayopakana na taifa jirani la Uganda.

ree

Mataifa ya Kenya, Somalia, Ethiopia. Eritrea na Djibouti yanakumbwa na hali mbaya zaidi ya nzige wa jangwani kwa miongo kadhaa. Nzige hawa wamevamia mataifa jirani ya Tanzania, Uganda na sasa Sudan Kusini.


Nzige wa jangwani wana uwezo wa kupaa kwa umbali wa kilomita 150 kwa siku. Kulingana na Umoja wa Mataifa, nzige wa jangwani wanakula chakula kingi kwa siku kuliko watu 35000 kwa kila kilomita moja mraba.


Uvamizi wa nzige hawa unafanya uhaba wa chakula kuwa mbaya zaidi katika eneo ambalo takriban watu milioni 25 wanateseka kufuatia miaka mitatu ya kiangazi na mafuriko.


Meshack Malo ambaye ni mwakilishi Sudan Kusini katika shirika la Chakula na Kilimo (FAO) amesema kwamba nzige hao tayari wamekomaa na wanatafuta mahali pa kutaga mayai ili kukuza kizazi kingine.

ree

Angalau nzige 2000 wamevuka mpaka wa Sudan Kusini. Katika kipindi cha miezi mitatu ya kuangua mayai, nzige mmoja anaweza kuzalisha nzige 20 zaidi. Suala kama hili husababisha nzige wengi kuzalishana na kuhatarisha mimea katika maeneo mbalimbali.


Taifa la Sudan Kusini lenye utajiri wa mafuta linapata nafuu ya mapigano ya miaka mitano ambayo yalisababisha ukame nchini humo mwaka wa 2017 na kusbabisha robo ya raia wa taifa hilo kuhama makwao.


Mwezi Disemba, shirika la chakula duniani lilisema kwamba hali ya chakula ilikuwa mbaya zaidi baada ya mafuriko kuathiri zaidi ya watu milioni moja.


 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page