top of page

Siku mbili za ,maombolezi baada ya shambulio la kigaidi kuangamiza raia 36

Serikali ya Burkina Faso imetangaza siku mbili za maombolezi kote nchini kufuatia shambulizi la kigaidi katika vijiji viwili lililowaacha watu 36 wakiwa maiti. Hili ni shambulizi la hivi punde kutokea nchini humo.

Kwa mujibu wa waziri wa mawasiliano Remis Fulgane Dandjinou, “kundi la kigaidi lilivamia kijiji cha Nagrago siku ya jumatatu na kuwaua watu 32. Magaidi hao pia waliwaua watu wanne zaidi katika kijiji cha Alamou na kufikisha idadi ya waliofariki kuwa 36.” Watu watatu walijeruhiwa katika shambulizi hilo katika mkoa wa Sanmatenga.


ree

Matukio haya ya yamesababisha mamia ya watu kutoroka makao yao na kukita kambi katika mji wa Kaya.

Danjinou ameeleza kusikitika kwa serikali ya Burkina Faso kufuatia shambulizi hilo huku rais Roch Marc Christian Kabore akitangaza Jumatano na Alhamisi kama siku za kuomboleza.

Burkina Faso pamoja na mataifa jirani ya Mali na Niger, yamekuwa ikishuhudia mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa makundi ya kujihami kuanzia mwaka 2015, mwaka ambao matukio ya vita yalianza kushuhudiwa katika kanda ya Sahel.

Sehemu nyingi za maeneo kame zimeshuhudia mapigano huku visa vingi vikishuhudiwa katika mataifa yanayoendelea kukua. Isitoshe, makundi ya kigaidi yanatumia umaskini, dini na migawanyiko ya kikabila kama njia za kuwasajili wapiganaji.


ree

Kulingana na shirika la Armed Conflict Location and Event Data Project (ACLED), Burkina Faso ilishuhudia visa 570 vya makabiliano, huku idadi ndogo ya visa hivi ikitekelezwa na makundi ya kigaidi yakiwemo Ansural Islam, Jama’at Nasr al-Islam wal Muslimin (JNIM) na kundi la Islamic State katika maeneo ya Sahara (ISGS).

Serikali ya Burkina Faso imeanzisha mradi wa raia kushirikiana na vikosi vya usalama ili kukabiliana na mashumbulizi ya mara kwa mara.

Hapo jana, bunge la Burkina Faso kwa kauli moja lilipitisha sheria itakayoruhusu raia kujitolea kupigana na makundi ya kujihami.

Kulingana na stakabadhi zilizofikia baadhi ya vyombo vya habari, raia wa kujitolea wenya umri wa miaka 18 na zaidi watasajiliwa katika maeneo yao huku wakizingatia idadi ya watu katika maeneo hayo.

Watakaosajiliwa watapewa mafunzo ya kijeshi kwa siku 14, kisha wapewe silaha ndogo na vifaa vya mawasiliano.



 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page