top of page

Shirika la afya ulimwenguni laendeleza huduma za dharura kushughukia maradhi ya Ebola nchini DRC.

Hali hii ya dharura huenda ikamalizika chini ya miezi mitatu iwapo wataalam wa afya katika shirika hilo watashauri.


Shirika la afya ulimwenguni limeongezea muda zaidi wa kukabiliana na mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola katika taifa la kidemokrasia la Kongo. Shirika hilo linasititiza kuwa kupunguka kwa ripoti za ugonjwa huo zinaashiria maafa chanya.


Kulingana na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la afya Tedros Adhanom, “ ili mradi kuna kisa kimoja cha Ebola katika eneo lolote, basi eneo lote si salama.” Kwa sasa, eneo la mashariki mwa taifa la DRC.

ree

Tedros ameonyesha matumaini kuwa hali hiyo ya dharura huenda ikakamalizika kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo iwapo wataalam katika shirika hilo watashauri hivyo.


Mwezi Juli, mwaka uliopita, shirika hilo la afya lilitangaza kuzuka kwa maradhi ya Ebola kuwa “hali ya dharura kwa umma” iliyostahili msaada wa kimataifa. Suala hili liliipa WHO mamlaka ya kuzuia usafiri wowote kuelekea sehemu fulani nchini DRC.


Kulingana na Tedros, ni visa vitatu tu vya Ebola vimeripotiwa katika kipindi cha wiki moja.

ree

Kabla ya janga hili la Ebola kutangazwa kumalizika, ni sharti kusiwe na ripoti za visa vyovyote kwa siku 42.


Mwaka jana, hali ya dharura ilitangazwa baada ya mtu mmoja kupatikana na virusi vya Ebola katika mji mkuu wa mkoa wa Goma, hiki kikiwa kisa cha kwanza katika mazingira ya mjini.


Tukio la sasa la Ebola liliripotiwa kwanza Agosti 2018 huku zaidi ya watu 2300 wakiripotiwa kufariki mashariki mwa DRC; sehemu ambayo makundi kadhaa ya kujihami yanaendesha shughuli zake.

ree

Mkurupuko wa sasa ni mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu mwaka 2014, wakati ambao maradhi ya Ebola yalisababisha vifo 11000 haswa katika mataifa ya Guinea, Liberia na Sierra Leone.


Juhudi za kukabiliana na kuenea kwa maradhi ya Ebola zimezuiliwa na mashambulizi yanayolenga wahudumu wa afya na migogoro katika kanda ya mashariki mwa DRC.

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page