top of page

Mgonjwa wa mwisho wa Ebola atibiwa na kuweka hai matumaini ya kumaliza zoezi la matibabu nchini DRC

Virusi vya Ebola vimeangamiza watu 2,264, kuambukiza watu 1200 zaidi na kuorodheshwa miongoni mwa virusi hatari zaidi katika historia ya nchi hiyo.


Mgonjwa wa mwisho wa virusi vya Ebola katika taifa la Kidemokrasia la Kongo ametibiwa, hii ni kwa mujibu wa shirika la afya ulimwinguni (WHO). Shirka hilo linasema kwamba hatua hii inafufua matumaini ya kumaliza kipindi cha miezi 19 ya mkurupuko wa maradhi hayo nchini Kongo.

ree

Kutibiwa kwa mgonjwa huyo kutoka hospitali moja katika mji wa mashariki wa Beni, kunaashiria mara ya kwanza ya virusi vya Ebola kutokuwepo tangu kutangazwa kwa mkurupuko wa virusi hivyo mwezi Agosti, mwaka 2018.


Katika kipindi hicho, virusi vya Ebola vimesababisha vifo 2,264 na maambukizi 1200 zaidi. Suala hili linaorodhesha mkurupuko huu wa Ebola miongoni mwa visa vibaya zaidi katika historia. Katika kipindi cha mwaka 2013-2016, virusi vya Ebola viliangamiza zaidi ya watu 11000 katika kanda ya Afrika Magharibi.


Taifa la Kidemokrasia la Kongo kwa sasa limeshihudia siku 14 bila visa vyovyote vipya vya maradhi ya Ebola kuripotiwa. Maradhi ya Ebola yanaweza kutangazwa kumalizika iwapo siku 42 zitapita bila visa vyovyote kuripotiwa.

ree

Baada ya kupokea cheti cha manusura, Semida Masika ambaye ni mgonjwa aliyepata matibabu alisema kwamba alifurahi sana kupata nafuu nyumbani. Masika alisema kwamba, “kama nusura wa mwisho, namshukuru Mungu na kumpa sifa.”


Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanon Ghebreyesus amesifu hatua hiyo huku akiitaja kuwa “nzuri zaidi, si kwangu tu, bali kwa ulimwengu mzima.” Tedros alizungumza haya katika kikao na wanahabari.


Hata hivyo, msemaji wa WHO ameonya kwamba ugonjwa wa Ebola bado haujamalizika huku akitaja ugumu wa kukabiliana na visa vya Ebola katika mashariki ya DRC kutoka na visa vya mapigano yananvyosababishwa na makundi yaliyojihami.

ree

Tarik Jasaveric, ambaye ni msemaji wa WHO alisema kwamba “kufuatia hali ngumu ya usalama, maambukizi ya Ebola katika makundi ambayo hayajafikiwa na wahudumu wa afya hayawezi kupuuzwa.” Tarik alisema kuwa kisa kimoja tu cha maradhi hayo huenda kikasababisha maambukizi mengi sana.


Hata ingawa visa vya Ebola vinazidi kushuka, suala hili linaonekana kupitwa na maambukizi ya Coronavirus ulimwenguni. Shirika la WHO linaamini kwamba kuenea kwa maradhi ya Coronavirus kunasababisha hali ya dharura ya afya ulimwenguni.


Kisa cha sasa cha Ebola nchini DRC ni cha 10 tangia mwaka 1976. Kuwepo kwa misitu mikubwa nchini DRC kunakisiwa kuwa hifadhi asili ya maradhi hayo.


 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page