top of page

Mgogoro na COVID kusababisha maafa ya njaa nchini DRC, Umoja wa Mataifa waonya

Mashirikaya Umoja wa Mataifa yasema kwamba DRC ina idadi kubwa zaidi ya watu ulimwenguni wenye mahitaji ya chakula cha dharura.


Watu milioni 27.3 nchini DRC wanakabiliana na njaa kali. Hii ni sawaia na thuluthi ya idadi ya jumla ya raia wa taifa hili. Kulingana na Umoja wa Mataifa, baa hili la njaa linatokana na migogoro na maafa ya kiuchumi ya COVID katika taifa hili.


Katika kikao cha pamoja, Shirika la Chakula ulimwenguni (WFP) na lile la Chakula na Kilimo (FAO) yalisema kwamba, DRC ina idadi kubwa zaidi ya raia wenye mahitaji ya chakula cha dharura ulimwenguni.

ree

Kando na migogoro na janga la Corona, idadi ya watu kwa sasa iko juu ikilinganishwa na takwimu za hapo awali kwa kuwa watu wengi waliangaziwa.


Kulingana na mwakilishi wa WFP nchini DRC Peter Musoko, utafiti wa sasa kwa mara ya kwanza uliangazia idadi kubwa ya watu na kuonyesha hali halisi ya mamilioni ya watu walio na mahitaji ya chakula. Musoko aliongezea kuwa taifa la DRC linastahili kulisha raia wake. Vilevile, alikashifu matukio ya watoto kulala njaa na jamii nyingi kukosa lishe.

Shirika la WFP limesema kwamba linahitaji dola milioni 662 mwaka huu ili ili kuzuia mamilioni ya raia kufikia kiwango cha kuitisha misaada ya chakula.


ree

Maafa ya migogoro


Maeneo yiliyoathiriwa sana na maafa na migogoro ni yale yaliyoko kwenya mikoa ya mashariki kama vile Ituri, Kivu Kaskazini, Tanganyika na mkoa wa kati wa Kasai. Maeneo haya yote yamekumbwa na migogoro mbalimbali. Raia waliotoroka mapigano katika maeneo haya walirejea na kupata mimea yao imeharibiwa.


Vita vya kujihami vimekuwepo nchini DRC kwa miongo kadhaa, haswa katika maeneo ya mashariki yanayopakana na mataifa ya Burundi, Rwanda na Uganda. Hali hii ingalipo hata baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kumalizika rasmi mnamo mwaka 2003.


Mashirika ya Umoja wa Mataifa yasema kwamba DRC ina idadi kubwa zaidi ya watu ulimwenguni wenye mahitaji ya chakula cha dharura.


 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page