Mataifa 37 ya Afrika yatangaza kuunga mkono tiba ya virusi vya Corona nchini Madagacar
- Moses Wangwa
- May 12, 2020
- 2 min read
Kufikia sasa, mataifa 37 barani Afrika yametangaza kuunga mkono tiba ya virusi vya Corona iliyopatikana nchini Madagascar. Idadi hii ni zaidi ya nusu ya mataifa 54 yanayopatikana barani Afrika.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya viongozi wa Afrika waliandaa mkutano na rais wa Madagascar Andry Rojoelina kupitia mitambo ya video kujadiliana kuhusiana tiba hiyo na kumhakikishia uungaji mkono kufuatia ugunduzi wa kipekee nchini Madagascar.

Baadhi ya viongozi waliofanya mkutano huo ni pamoja na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Afrika, Rais Abdul Fatah El Sisi wa Misri, Rais Felix Tshisekedi wa DRC, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Mahamadou Issoufou wa Niger, Rais Idris Derby wa Chad, Rais Boubacar Keita wa Mali na Rais Andry Rojoelina wa taifa la Madagacar.
Baada ya hakikisho hili kutoka kwa mataifa ya Afrika, kiongozi wa Madagascar amehawahakikishia viongozi wengine kuwa dawa hiyo itafikia mataifa yote ya Afrika katika kipindi cha siku chache zijazo ili kusaidia kukabiliana na janga la virusi vya Corona.
Taifa la Madagascar limeanza shughuli za ujenzi wa viwanda zaidi vitakavyosaidia kutengeneza dawa hiyo kwa kiasi kikubwa na kuhakikisha kwamba taifa hilo litatimiza mahitaji ya mataifa mbalimbali.

Kwa sasa, dawa hiyo imepewa jina la Covid-Organic na imetengenezwa kutoka kwa mmea wa artimisia annua; mmea ambao huzalisha dawa ya kutibu ugonjwa wa malaria. Kulingana na Rais Rojoelina, kiwanda kinachojengwa kinatazamiwa kuanza oparesheni katika kipindi cha mwezi mmoja. Rais huyo aliongezea kwamba “watafiti na wanasayansi nchini humo wanafanya kila wawezalo ili kufanya dawa hiyo kufikia viwango vinavyostahili.”
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alisema kwamba “atatuma ndege nchini Madagascar kuleta dawa hiyo." Kupitia mtandao wake wa Twitter, Rais Rojoelina alisema kwamba naibu wa waziri wa afya nchini Equatorial Guinea alikuwa amewasili nchini Madagascar kununua dawa hiyo kwa kiwagno kisischojulikana. Baadhi ya mataifa ambayo yameonyesha ari ya kununua dawa ya Covid-Organics ni pamoja na Senegal, Guinea-Bissau na Comoros.
Agizo la WHO
Shirika la afya ulimwenguni WHO limeagiza majaribio ya kliniki ya Covid-Organics; ambayo ni kinywaji cha mitishamba kinachosemekana kuzuia na kutibu wagonjwa wanaougua virus vya Corona.

Kulingana na mkurugenzi wa WHO katika kanda ya Afrika Matshidiso Moeti, “shirika hilo linahimiza serikali ya Madagascar kushirikiana na WHO.” Moeti alisema haya katika kikao na wanahabari.
Vilevile. Moeti ametahadharisha mataifa dhidi ya kununua dawa ambayo haijafanyiwa majaribio ya kliniki. Kuligana na Moeti, majaribio ya kliniki yatahakikisha usalama na ufanisi wa dawa hiyo
Comments