top of page

Makali ya njaa yanaposhuhudiwa, ni nani atakayewalinda watoto dhidi ya biashara ya ngono?

Wasichana wadogo katika kanda ya Afrika Kusini wanashiriki biashara ya ngono ili kuepuka janga la njaa linaloathiri mamilioni ya watu katika maeneo hayo. Hii ni kulingana na mashirika ya kutoa misaada.

Shirika la World Vision linasema kwamba wasichana wa wa umri wa miaka 12 wanauza miili yao kwa hadi shilingi 40 ili waweze kulisha familia zao. Taifa la Angola linashuhudia ukame mbaya zaidi kwa kipindi cha miongo minne.

ree

Umoja wa Mataifa unasema kwamba watu milioni 45 katika kanda ya Afrika Kusini wamekumbwa na baa la njaa linalosababishwa na ukame, mafuriko makubwa na migogoro ya kiuchumi.

Robert Bulten ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya dharura katika shirika la World Vision alisema kwamba “wasichana wadogo wanalipwa shilingi mia moja kwa kushiriki ngono; pesa ambazo zinatosha kununua kilo mbili za unga wa ugali.’’ Alidhibitisha kuwa wasichana wanaoshiriki ngono ni wenye umri wa kati ya miaka 12 na 17.

Bulten aliongezea kuwa bei ya bidhaa za kimsingi zimeongezeka mara dufu na akatabiri hali kuwa mbaya zaidi ikizingatiwa kwamba kipindi cha kuvuna kinatarajiwa kuanza mwezi Juni.

ree

Nchini Zimbabwe, shirika la kimataifa la CARE lilisema kwamba ripoti zinaonyesha wasichana wa miaka 14 wanashiriki ngono haswa wanapoelekea taifa jirani la Afrika Kusini na karibu na migodi ya dhahabu.

Kulingana na mtaalamu wa masuala ya kijinsia katika kanda hiyo Everjoy Mahuku, “wakati mwingine wasichana hao hulipwa takriban shilingi 31 wanaposhiriki ngono, suala linaloashiria hali mbaya zaidi.”

Mshauri wa shirika la Action Aid katika kanda ya Afrika Kusini Chikondi Chabvuta alisema kuwa wanawake na wasichana wanalazimika kushiriki biashara ya ngono ili wajikimu kimaisha nchini Mozambique na Malawi.

Mataifa mengine yanayoathiriwa na hali hii ni pamoja na Zambia, Madagascar, Namibia, Lesotho na Eswatini. Wafanyikazi wa mashirika ya misaada wanasema kwamba wengi wa wasichana wanaoshiriki ngono wanastahili kuwa shuleni. Hata hivyo, wasichana hawa wamelazimika kuacha shule kufuatia umaskini unaokita mizizi na kufungwa kwa shule nyingi katika maeneo hayo.

Waischana wadogo wanakumbwa na hatari ya kubakwa wanapotembea masafa marefu kutafuta maji. Kulingana na Bulten, familia zinazong’ang’ana kupata mahitaji ya kimsingi zinalazimika kuwaoza binti zao wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mahitaji ya chakula. Vilevile, baadhi ya familia zinafanya hivyo ili kuzuia mabinti wao kushiriki ukahaba.

Kulingana na shirika la kimataifa la Msalaba mwekundu, janga hili limesababisha ongezeko la kuozwa kwa watoto nchini Zimbabwe, Zambia, Lesotho na Namibia.


 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page