top of page

Mahakama ya Burundi yawafunga wanahabari wanne kwa ‘kudhoofisha usalama wa kitaifa’

Wanahabari hao wanafanya kazi na shirika la utangazaji la Iwacu,ambalo ni moja kati ya mashirika machache ya kibinafsi yaliyosalia nchini Burundi.

Mahakama moja nchini Burundi imewahukumu wanahabari wanne kifungo cha miaka miwili na nusu gerezani kwa madai ya kudhofisha usalama wa nchi.

Wanne hao walikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana katika wilaya ya Musigati, mkoa wa Bubanza ulioko magharibi mwa nchi ya Burundi. Wanahabari hao wanasemekana kupeperusha hewani hafla ya waasi kutoka mkoa wa Kivu kusini nchini DRC.

Upande wa mashtaka uliomba mahakama kuwafunga kwa miaka 15 kufuatia mawasiliano kwenye mtandao wa Whatsapp kati ya wanahabari hao na mmoja wao anayeishi mafichoni. Ujumbe huo ulinakiliwa ukisema kwamba “tunaelekea Bubanza…kuwasaidia waasi.

Wanahabari hao wanafanya kazi na shirika la utangazaji la Iwacu,ambalo ni mojawapo ya mashirika ya utangazaji ya kibinafsi yaliyosalia nchini humo.

Mwanzilishi wa shirika la Iwacu Antoine Kaburahe anayeishi mafichoni nchini Ubelgiji alisema kuwa shirika lake litakata rufaa kufuatia uamuzi wa mahakama kuwapa kifungo wanahabari hao. Kaburahe alisema haya kupitia mtandao wa twitter. Shirika hilo lina hadi siku 30 kukata rufaa.

Seif Magango, ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Shirika la kimatifa la Amnesty katika kanda ya Afrika Mashariki alisema kwamba “hukumu na kifungo cha Agnes Ndirubusa, Christine Kamikazi, Egide Harerimana na Torence Mpozenzi kwa kesi isiyokuwa na msingi inaashiria siku ya huzuni na kukiuka uhuru wa kujieleza na ule wa vyombo ya habari nchini Burundi.”

Magango amesisitiza kwamba mahakama “lazima itupilie mbali uamuzi huo” na wanahabari hao “kuachiliwa huru haraka iwezekanavyo.

Itakumbukwa kwamba mwanahari wa shirika la Iwacu Jean Bigirimana aliyetoweka mwaka 2016 hajapatikana hadi sasa.

Vizuizi katika vyombo vya habari

Serikali ya Burundi imewekea vizuizi vyombo vya habari wakati ambao taifa hilo linajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi Mei.

Kufikia sasa, stesheni nyingi za redio na mashirka ya utangazazaji yamefungwa na kuwalazimisha wanahabari wengi kukimbilia mataifa salama.

Serikali ya rais Pierre Nkurunzinza imezuia mashirika ya Sauti ya Marekani na BBC kupeperusha habari kutoka nchini Burundi.

ree

Burundi imekumbwa na hali mbaya ya migogoro ya kisiasa tangu mwaka 2015 pale ambapo rais Nkurunzinza alitangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu. Nkurunzinza aliibuka mshindi katika uchaguzi, suala lilisababisha maandamano makubwa kufanyika kote nchini kupinga uchaguzi huo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 1200 wameuawa katika malumbano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji.


ree

Rais Nkurunzinza alitangaza kwamba hatawania kipindi kingine mamlakani na chama tawala kikamteua jenerali wa jeshi Evariste Ndayishimiye kama mgombeaji urais katika uchaguzi wa mwezi Mei.

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page