top of page

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yasababisha vifo vya watu 13 mjini Kigali

Watu 13 wamethibitishwa kufariki katika mji mkuu wa Rwanda kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha. Kulingana na maafisa wa serikali, 13 wameaga dunia na wengine kujeruhiwa kufuatia hali hiyo.

Mvua kubwa inayoshuhudiwa ilianza kunyesha jumapili usiku na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosomba nyumba 15 na kuharibu baadhi ya barabara

ree

Kulingana na msemaji wa wizara inayosimamia majanga nchini Rwanda Claude Tuyishime, wizara hiyo inaweka idadi ya walioga dunia kuwa 13 kwa sasa. Tuyishime aliongezea kuwa “baadhi ya miili ya watu walioripotiwa kutoweka imepatikana na upelelezi unaendelea.”

Mnamo January 28, mvua kubwa nchini Rwanda ilisababisha vifo vya watu watatu. Vilevile mvua hiyo iliharibu mazao ya shambani na kusomba makaazi ya watu. Mwezi Disemba mwaka jana, watu 12 waliangamia mjini Kigali kufuatia mvua kubwa. Maafisa wa serikali wanasema kwamba zaidi ya makaazi 100 yameharibiwa.

ree

Serikali ya Rwanda imeanzisha shughuli za uhamishaji kwa wakaazi wa nyanda za chini na maeneo mengine yasiyo salama.

Idara ya hali ya anga nchini Rwanda imesema kwamba mvua zaidi inatarajiwa. Mji wa Kigali na maeneo ya kaskazini mwa Rwanda yako katika nyanda za juu na huwa na hatari ya maporomoko ya ardhi katika msimu wa mvua.

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page