top of page

Kisa cha kwanza cha Coronavirus barani Afrika kimethibitishwa nchini Misri.

Wizara ya afya nchini Misri inasema kwamba muathiriwa ni wa asili ya kigeni na ametengwa na kulazwa hospitalini.


Misri imethibitisha kisa cha kwanza cha ugonjwa hatari wa Coronavirus uliotokea nchin China mwishoni mwa mwaka jana. Kufikia sasa, ugonjwa wa Coronavirus umeenea kwa mataifa mbalimbali kote ulimwenguni.


Kulingana na msemaji wa wizara ya afya nchini Misri Khaled Mugahed, “aliyeathiriwa ni raia wa kigeni na hajaonyesha dalili zozote mbaya.”

ree

Maafisa wa afya walifanikiwa kuthibitisha kisa cha ugonjwa huo kufuatia mpango uliotekelezwa na serikali unaofuatilia wasafiri wanaotoka mataifa ya kigeni haswa yale ambayo visa vya Coronavirus vimeripotiwa.


Taarifa kutoka kwa wizara hiyo zinasema kwamba mtu aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo amelazwa hospitalini. Hata hivyo, wizara ya afya haijaeleza wazi uraia wa mgonjwa huyo na mahali alipoingilia nchini.


Tukio hili limefanya Misri kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuthibitisha kisa cha Coronavirus. Vilevile, Misri ni ya pili katika kanda ya mashariki ya kati kuthibitisha kisa cha Coronavirus baada ya Falme za Kiarabu (UAE) iliyothibitisha kisa cha kwanza mwezi uliopita.


ree

Kwa jina rasmi, ugonjwa huu unajulikana kama COVID-19, na virusi vya ugonjwa huu viligunduliwa Wuhan ambao ni mji mkuu katika mkoa wa Hubei nchini China.


Kufikia sasa, ugonjwa wa Coronavirus umesababisha vifo 1400 huku takriban watu 65000 wakiambukizwa ugonjwa huo kote duniani.


Zaidi ya mataifa ishirini yamethibitisha visa vya Coronavirus na mataifa mengi kuwaondoa raia wao kutoka mkoa wa Hubei.


Shirika la afya ulimwenguni limeonya kwamba virusi vya Coronavirus “ni tishio kubwa” kwa dunia.

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page