top of page

Hospitali iliyojengwa kwa siku kumi nchini China yaanza kuwahudumia wagonjwa.

Vyombo vya habari nchini China vinasema kwamba hospitali mpya iliyojengwa katika mji wa Wuhan ilianza kupokea wagonjwa hapo jana. Hospitali spesheli ya Huoshenshan ilijengwa ili kuwashughulikia wagonjwa walioathiriwa na maradhi ya Coronavirus ambayo kufikia sasa yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 300 na maelfu kuambukizwa.

Hospitali ya Wuhan iliyo na vitanda vya wagonjwa 1000 ilijengwa ili kuwapa matibabu wagonjwa wa Coronavirus. Vilevil, hospitali hii imesaidia pakubwa kukabiliana na uhaba wa vitanda vya wagonjwa katika hospitali zingine jijini Wuhan. Dalili za kwanza za Coronavirus zilishuhudiwa jijini Wuhan mwishoni mwa mwaka 2019 hivo kufanya jiji hili kuwa chanzo cha maradhi hayo.

Kufikia sasa, maradhi ya Coronavirus yamesababisha vifo 361 nchini China na maambukizi 17000 nchini humo. Vilevile, visa 171 vya maambukizi ya Coronavirus vimeripotiwa katika sehemu zingine ulimwenguni.

Zaidi ya wafanyikazi 7500 walihusika katika ujenzi wa hospitali ya Huoeshenshan. Serikali ya China inajenga hospitali nyingine jijini Wuhan itakayokuwa na vitanda 1600 na kusaidia kukabilian na maradhi ya Coronavirus. Hospitali hii inatazamiwa kumalizika wiki hii.

Wagonjwa wa kwanza walilazwa katika hospitali ya Huoshenshan hapo jana asubuhi.


 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page