top of page

COVID-19: Kenya miongoni mwa mataifa yanayotazamiwa kufanyiwa majaribio ya chanjo ya covid -19

Matumaini ya kupata chanjo ya covid-19 yamepata msukumo mkubwa baada ya majaribio ya kliniki kuonyesha maendeleo makubwa.


Chanjo ya ChAdOx1 nCoV-19 - ambayo imetengenezwa na kampuni ya AstraZeneca ikishirikiana na chuo kikuu cha Oxford - inaonyesha matokeo ya kutia moyo katika hatua ya mwisho ya majaribio ya kliniki.

ree

Kulingana na afisa mkuu mtendaji wa AstraZeneca Pascal Soriot, “utengenaji wa chanjo unaendelea vyema na kuna habari za kuridhisha kufikia sasa.” Soriot aliongezea kwamba kampuni hiyo inahitaji kuonyesha ufanisi katika majaribio ya kliniki.


DOZI BILIONI MBILI


Kampuni ya AstraZeneca imeshirikiana na mataifa mengi kutengeneza zaidi ya dozi bilioni mbili za chanjo ya covid-19 inayosababisha kinga mara mbili kwa watu walio na umri wa kati ya miaka 18 na 55.


Majaribio ya kliniki ya chanjo ya ChAdOx1 nCoV-19 yanatazamiwa kuanzishwa nchini Kenya, ambayo ni mojawapo ya maeneo ya majaribio. Vilevile, Kenya ni mojawapo ya mataifa ya Afrika yalioathiriwa na virusi vya corona. Utafiti zaidi unaendelea katika mataifa ya Afrika Kusini na Uingereza. Nchini Brazil, chanjo hiyo imefikia hatua za mwisho za majaribio ya kliniki.

ree

Wakati huo huo, Russia imetangaza kuwa inanuia kuwapa chanjo madaktari na walimu kutumia dozi za kwanza za chanjo ambayo imetengeneza.


Waziri wa afya nchi Russia Mikhail Murashko amenukuliwa akisema kuwa zoezi hili litatekelezwa kufikia mwisho wa mwezi Agosti, huku chanjo za umma zikitekelezwa mwezi Oktoba.


Majaribio ya mapema ya chanjo iliyotengenezwa na taasisi ya Gamaleya ilikamilika mwezi uliopita na chanjo hiyo inasajiliwa.


CHANJO 160 ZA COVID-19


Nchini Marekani, Dakatari Anthony Fauci ambaye ni mkurugenzi wa taasisi ya kitaifa inayokabiliana na magonjwa ya kuambukiza alisema kwamba chanjo ya virusi vya corona itakuwa tayari kwa raia wa Marekani kufikia mwanzo wa mwaka 2021.

ree

Kufikia sasa, kuna zaidi ya chanjo 160 za covid-19 duniani zinazotengenezwa huku nyingi kati ya chanjo hizo zikiwa katika hatua za kwanza za majaribio


Huku umakini mkubwa ukiwekwa kwenye utengenaji wa chanjo ya covid-19, kuna majaribio mengine ya dawa zinazoweza kutumiwa kutibu covid-19. Taifa la Kenya linafanyia majaribio dawa ya remdesivir (kutoka shirika la WHO) na tocilizumab. Lengo la majaribio haya ni kutumia dawa hizo kama chanjo iwapo matokeo yatakuwa ya kuridhisha.



Pata habari zaidi za humu nchini na kote ulimwenguni kwa kubonyeza hapa.

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page