top of page

Kero la ugaidi latikisa Afrika

Updated: Jan 11, 2020

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika magharibi ya Afrika na eneo la Sahel umesema kwamba sehemu hiyo “imeshuhudia ongezeko baya la mashambulizi ya kigaidi yanayolenga raia na walinda usalama.

Mohamed Ibn Chambas alieleza Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hapo jumatano kwamba “mashambulizi ya kigaidi ambayo hayajawahi kushuhudiwa” yamesababisha hofu kati ya raia wa maeneo hayo.

Alisema kuwa mashambulizi yameongezeka mara tano katika mataifa ya Burkina Faso, Mali na Niger tangu mwaka 2016 huku zaidi ya vifo 4000 vikiripotiwa mwaka 2019 pekee ikilinganishwa na vifo 770 miaka mitatu iliyopita.

Chambas alisisitiza kuwa “kwa kiwango kikubwa, malengo ya mashambulizi ya kigaidi yamebadilika kijiografia na kuelekea upande wa mashariki kutoka Mali kuelekea Burkina Faso, na yanaendelea kutishia mataifa ya magharibi ya Afrika yanayopakana na bahari ya Atlantic”

ree

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulisema kwamba mashambulizi hayo mara nyingi huwa “mbinu makusudi ya makundi ya kigaidi kuthibiti barabara za silaha na zile za ulanguzi” na kujihusisha katika shughuli haramu ikiwemo uchimbaji madini ili kuendeleza oparesheni zao.

Kati ya mashambulizi ya hivi karibuni ni shambulio la kombora siku ya Alhamisi katika kampi ya kijeshi kaskazini ya Mali ambapo watu 20 walijeruhiwa miongoni mwao wakiwa walinda usalama 18 wa Muungano wa Mataifa. Hii ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa nchini Mali.

Kulingana na wakaazi na habari za majeshi, takriban majeshi 20 waliuawa na watu 1000 kulazimika kukimbilia maeneo salama Jumanne jioni kufuatia shambulizi katika mji mmoja wa jimbo la Borno, kaskazini mwa Nigeria.

Shambulizi lingine lilitokea jumatatu pale ambapo bomu lililotegwa kando ya barabara kulipuka na kuwaua zaidi ya majeshi watano. Tukio hili lilifanyika katika eneo la Alatona karibu na mpaka wa Mali na Mauritania. Zaidi ya majeshi 140 wa Mali wamewauwa katika mashambulizi tangu mwezi Septemba.

Siku ya Jumamosi, bomu lilitogwa kando ya barabara nchini Burkina Faso lililipuka na kuangamamiza watu 14. Miongoni mwa waliofariki ni watoto saba na wanawake wanne.

Katika mkesha wa krismasi, raia 35, wengi wao wakiwa wanawake waliaga dunia kufuatia shambulizi katika kambi ya kijeshi katika mkoa wa Soum, kaskazini mwa Burkina Faso.

Chambas alisema kuwa mashirika ya kiserikali, mashirika ya kikanda na jamii ya kimataifa yanahamisisha ili yakabiliana na utovu wa usalama Magharibi mwa Afrika na maeneo ya Sahel.

ree

Chambas amewahimiza viongozi katika maeneo hayo kutimiza ahadi zao za kukabiliana na ugaidi huku akisema kwamba “sasa ndio wakati wa kuchukua hatua”

Katika ripoti yake kwa Baraza la usalama mwezi Juli, mtaalamu mmoja wa Umoja wa Mataifa alisema kwamba “hatua kuu za kimataifa katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2019 ilihusisha ari ya kukabiliana na makundi ya kigaidi maghaibi mwa Afrika, ambapo wapiganaji kutoka ISIL na Al Qaeda wanakula njama kudhoofisha mataifa dhaifu.

Chambas alisema kuwa mashambulizi ya kigaidi mara kwa mara yanaunganika na uhalifu uliopangwa na vita baina ya makundi yanayoshindana.

Ikizingatiwa kwamba takriban asilimia 70 ya idadi ya watu wa Magharibi ya Afrika wanategemea kilimo na ufugaji, makabiliano kati ya wakulima na wafugaji “yanasalia kuwa mojawepo ya chanzo cha vurugu katika eneo hilo”

Chambas alisema kuwa katika miezi michache ijayo, mataifa sita ya Magharibi ya Afrika yatachagua viongozi wao katika uchaguzi wa kidemokrasia.


Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 711812075

©2019 by Afrikana. Proudly created with Wix.com

bottom of page